Sunday 24th September 2017 Taarab Queen Bi Shakila dies at 71 | MsimuliziOnline.Com

Support Us

  • Users online: 1 
  • Visitors today : 86
  • Total visitors : 94,808

Msimulizi Social Media Channels

Taarab Queen Bi Shakila dies at 71

Shakila Saidi gwiji katika muziki wa taarabu amefariki.

Muimbaji taarab maarufu nchini Tanzania, Shakila Saidi amefariki dunia Ijumaa nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar es Salaam.

Bi Shakila ambaye alianza kuimba taarab mwaka 1961, alivuma sana katika uwanja wa taarabu mkoani Tanga ambao aliimba katika bendi ya Lucky Star na Black Star. Katika miaka 1980 alijiunga na bendi ya JKT na kujizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki na Kati. Alistaafu kuimba katika taarabu kwenye bendi hiyo mwaka 1990.

Atakumbukwa kwa nyimbo zake maarufu ambazo zilizokuwa na ujumbe mzito sana kama “Kitumbiri”, “Mapenzi yamepungua” na ” Macho yanacheka.”

Bi Shakila aliolewa mwaka 1960 akiwa na umri wa miaka 11. Amejaaliwa watoto 13 na wajukuu kadhaa. Atakumbukwa kwa ucheshi wake na mara nyingi alikuwa akialikwa kutumbuiza kwenye sherehe mbali mbali za harusi hasa mjini Dar es Salaam na Tanga.

Mungu ailaza roho yake mahali pema peponi. Ameen.

Source: VOA

READ  Top 5 Bi Shakila's all time Taarab hits

 

About the author

Msimulizi

Publisher and Editor in chief MsimuliziOnline, community news and information hub serving East African-Canadians.

Be the first to comment

Leave a comment

Your email address will not be published.


*


}