Loblaws Yazindua Tovuti la Usajili wa ‘$25 Gift Card’ za Mkate wa Bofulo

Tarehe yako ya kuzaliwa na anuani  yako ya barua pepe ni miongoni mwa vile vitavyohitajika ili upate $25 Gift Card kama fidia ya kupandisha bei ya mkate kiholela Loblaws.

Kwanzia wiki hii (J’tatu, Januari 8, 2018) unaweza kujiandikisha kwenye website maalum ya Loblaws ili kupata $25 Gift Card kama fidia kutoka supermarket hiyo, ambayo imekiri kuongeza bei ya mkate  kiholela kwa zaidi ya miaka kumi.

Supamarket hiyo kubwa nchini Kanada pia imesema wale watakaoandikisha kupata Gift Card hizo hawatozuiliwa kuishitaki suparmarket hiyo katika siku zijazo.

Kesi kadhaa zimefunguliwa mahakamani didhi ya Loblaw Companies Ltd tangu supermarket hiyo kukiri mwezi wa Desemba 2017  kuwa pamoja na supermarket nyinge zilikua zikipandisha kiholela bei ya mkate wa bofulo kwa  miaka 14.

Aina ya mikate ambayo inadaiwa  kuongezwa bei ni:

 • Ben’s Bread.
 • Bon Matin Bread.
 • Country Harvest Bread.
 • Dempster’s Bread.
 • D’Italiano Bread.
 • Gadoua Bread.
 • McGavin’s Bread.
 • No Name Bread.
 • Old Mill Bread.
 • POM Bread.
 • Weston Bread.
 • Wonder Bread.

Mkaazi yeyote yule aliyewahi kununua mkate kutoka Loblaws, No Frills, Superstore, Provigo, Zehrs na supermarket zingine zenye uhusiano na Loblaws kati ya mwaka 2002-2015 anaweza kujiandikisha kupata $25 GiftCard bila ya kuonesha risiti ya kununua mkate kwenye supermarket za Loblaws.

Go to the Loblaw Card Program website (www.loblawcard.ca) and enter your email address. This will ensure you receive a notice once registration opens on Jan. 8.

-Msimulizi

 

  About Msimulizi

  Publisher and Editor in chief MsimuliziOnline, community news and information hub serving East African-Canadians.

  View all posts by Msimulizi →

  Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *