Kanada kuanza kuuza bangi kwanzia Julai Mosi, pia itaruhusu miiche minne kwa kila nyumba

Chama tawala cha nchini Kanada, The Liberal Party of Canada leo kimepeleka musuada wa kuhalaisha bangi katika bunge la nchi hiyo ya Marekani ya magharibi.

Musuada huo  ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu sana tangu kampeni za uchaguzi mwaka 2015, ambapo Liberals waliaahidi wananchi kuwa, kama wananchi watawachagua kuongoza nchi, pale waiingiapo madarakani watahalalisha uuzaji, uvutaji na ulimaji wa bangi nchini Kanada.

Musuada huo utaruhusu yeyote yule mwenye umri wa miaka 18, na kuendelea kuwa na gramu 30 za bangi bila ya kuwa na hatia ya kupatikana na madawa ya kulevya.

Watumiaji na wavuta bangi pia wanaweza kuotesha miiche minee majumbani mwao kwa ajili ya matumizi yao ya binafsi. Na wale wanaotaka kununua wataweza kufanya hivyo kutoka dispensary maalum za bangi kote Kanada.

Waziri wa sheria wa Kanada, Bi. Jody Wilson-Raybould alipokuwa akiongea na waandishi wa habari punde tu pale musuada huo kupelekwa bungeni, alisema “Leo ni siku muhimu sana.” Musuada hu unalida watoto na wakati huo huo utatokomeza biashara ya uuzaji wa bangi kiholela alisema bi Raybould.

Serikali inatarajia musuada huo kupitishwa bungeni na kuwa sheria ya nchi pale ifikapo July mosi, ambayo ni Canada Day, siku Kanada ilipopata mamlaka kamili kutoka Uingereza.

Polisi wamesema vifaa vya kupima mate vitatumika pale watapowashuku waendesha magari waliokuwa wamevuta bangi. Pia wataangalia macho na harufu.

Macho ya wavuta bangi mara nyingi hubadilika kuwa mekundu pale wavutapo andasi hiyo.

Soma zaidi hapa

 

About Msimulizi

Publisher and Editor in chief MsimuliziOnline, community news and information hub serving East African-Canadians.

View all posts by Msimulizi →

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *