Kamati ya Afya Bungeni kuifanyia utafiti sheria ya Utoaji damu wa Wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja

Kwa sasa Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao (men who have sex with men (MSM)) hawawezi kuchangia katika utoaji damu.

Wabunge kwenye kamati ya afya wamepitisha mswada leo Jumanne, itakayowaruhusu kutathmini sheria ambayo inakataza wachangiaji damu wanaume wanoshiriki katika mapenzi ya jinsia moja kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi wenzao Kanada.

Hivi karibuni (Mwezi wa Juni), Wizara ya Afya Kanada iliondoa vipingamizi kuchangia damu, kwa wanaume walioaacha au kujiepusha kufanya mapenzi na wanaume wenzao kwa muda wa mwaka moja. Lakini ni marufuku kwa wale wanaume ambao wanaendelea kufanya mapenzi ya jinsia moja. Hadi mwaka jana(2015) ilikuwa marufuku kwa MSM kuchangia damu kama hawajajiepusha na tabia hiyo kwa miaka mitano.

Kamati hiyo ya bunge itafanya tathmini ya kisayansi katika sheria inayopiga marufuku uchangiaji wa damu na itawaalika wataalamu ili kuaanda sera zitakato tumika hapo baadaye.

Kwa zaidi soma habari hii kutoka CBC

 

 

 

 

READ  Zanzibar Secession back in spotlight after anti-union activist seek day in East African courts

About Msimulizi

Publisher and Editor in chief MsimuliziOnline, community news and information hub serving East African-Canadians.

View all posts by Msimulizi →

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *