Donald Trump kuaapishwa kuwa raisi wa 45 wa Marekani (LIVE)

Leo Ijumaa January 20, 2017 ni siku ya mwisho kwa Rais Barak Hussain Obama kama raisi wa Marekani. Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa taifa hilo kubwa lenye nguvu ya kiuchumi na kijeshi duniani.

Hatua ya kwanza kabisa ya rais mteule Trump baada ya kuapishwa kuwa rais ni kupokea kisanduku chenye kodi ya kulipua bomu la nuklia, ambayo ataweza itumia iwapo Marekani itashambuliwa na taifa lingine duniani. Baada ya kupewa taarifa hiyo na makamanda wa kijeshi, Trump kama raisi atakuwa na dakika 30 kuaamua matumizi ya bomu la nuklia.

Siku ya leo ni hatua muhimu katika demokrasia, ya kungatuka madarakani kwa njia ya amani imekuwa ndio chanzo cha kifanya taifa la Marekani kuwa mfano mmoja wa kuiigwa na mataifa mengine.

Wabunge zaidi ya 50 wa chama cha Democratic katika Bunge la Congress watasusia sherehe za kuapishwa leo kwa Trump – ukiwa ni upinzani mkubwa wa kisiasa dhidi ya rais mpya –BBC

Baada ya utamaduni wa kunywa kahawa pamoja Rais Obama na Rais mteule Trump, ambaye ameahidi kufutilia mbali mswada wa afya na sheria iliyotungwa na rais Obama ijulikanayo kama Obamacare, amewaahidi wafwasi wake kuwa atajenga ukuta mpakani na meksiko na ataanzisha uandikishaji wa wahamiaji wa Kiislamu watakaoingia Marekani.

Tunakualika uwenasi kwa kipindi chote cha sherehe hizi za kuaapishwa kwa Trump kwa kuwa rais wa 45  a Marekani, siku muhimu kwa Trump, waMarekani na hasusan ulimwengu mzima.

baada ya sherehe hizo unaweza acha comment na kujiunga na wadau wengine wa Msimulizi kujadiali tukio hili la historia.

 

 

About Msimulizi

Publisher and Editor in chief MsimuliziOnline, community news and information hub serving East African-Canadians.

View all posts by Msimulizi →

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *